Na David John Mwanza
KIKUNDI
cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) wameiomba Serikali kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na umoja huo ambapo wameamua kwa dhati
kupambana na umasikini kwa vitendo.
Wamesema
wao kama kikundi cha ujasiliamali wilaya ya ilemela kimebeba vikundi
zaidi ya 16 ambapo wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za
ujasilimali ikiwamo ufundi nguo,Mapambo nakadhalika.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi leo Katka ofisi za kikundi hicho Mwenyekiti
wake Asile Amour.Amesema kikundi hicho kimeazishwa Mapema mapema mwaka
huu na kimekusanya zaidi ya vikundi 16kutoka katika Kata ya Nyasaka
wilayani Ilemela.
"Tunaiomba
Serikali kutuunga mkono kwani tumeamua kwa dhati kuunga mkono serikali
hususani katika sera yake ya viwanda kuona na sisi kama wanawake
tunajikomboa. "amesema Mwenyekiti Asile
Amesema
wamejipanga kufanya harambee kwa lengo la kutunisha mfuko wao huku
akitoa rai kwa viongo wa vyama na Serikali kushiriki kuwaunga mkono kama
wanavyofanya kwenye maeneo mengine.
Naye
Mhazini wa kundi hilo Esther Kakwene amesema kundi lao lina wanachama
zaidi ya 100 nikundi kubwa ambalo limekusanya watu kutoka kila mtaa
ndani ya kata ya Nyasaka.
"Hapa
tulipo tumepewa sehemu ya kujenga Ofisi kwa ajili ya kikundi chetu
hivyo tunaomba viongozi wetu watusaidie ili tufanikishe malengo yetu.
Kundi hili tumesajiliwa na tumepewa cheti cha utambulisho hivyo tupo
kikazi zaidi. Amesema Esther.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...