VIFIJO
na ndelemo vilivyochangamana na majozi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo ya shule ya msingi 2017 katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la
Wokovu jijini Dar es Salaam leo.
Furaha
iliyoje kwa watoto waliohitimu masomo ya msingi na majozi kwa
waliobakia, ikiwa risala ya wahitimu imetoa changamoto mbalimbali kwa
watoto wenye ulemavu ikiwemo vifaa visaidizi kwa watoto hao pamoja na
mafuta ya kupaka kwa watoto wenye ulemvu wa ngozi(Albino).
Akizungumza
katika mahafali hayo jijini Dar es Salaam leo, Mwalimu wa Michezo
katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Emmanuel Ibrahim ameiomba
serikali kuwaruhusu watoto hao wenye ulemavu na wanavipaji mbalimbali
washiriki mashindano ya Kitaifa pamoja na ya kimataifa kama watoto
wengine.
Pia
wameomba kuongezewa Madaktari watakaotoa huduma ya afya kwa watoto hao
wenye ulemavu ilikukidhi mahitaji ya watoto wenyeulemavu shuleni hapo.



wahitimu
wa shule ya msingi Jeshi la Wokovu na Watoto wenye ulemavu tofauti
tofauti wakitumbuiza ngojera mbele ya mgeni rasmi zilizokuwa na mahusia
mazuri kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu pamoja na kuwashuru walezi
na walimu wao kwa kuwalea tangu walipokuwa Darsa la kwanza mapaka sasa
wanahitimu masomo yao ya shule ya msingi.
Wahitimu wa Shule ya Msingi Jeshi la wokovu wakimsiliziza mgeni rasmi jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya kuwaaga.
Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...