Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika
kikao cha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kikao hicho cha siku
mbili kimeanza kufanyika mapema Septemba 15 katika UkumbiwaMikutano wa
Kimataifa (AICC) uliopo jijini Arusha
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji
kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana
katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa,
Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya
Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu,
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati.
Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wakiwa
katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi,
Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji
Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin
Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi.
Baadhi
ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
1.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika
Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni
kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano
wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye
nguzo namba mbili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati kutekelezeka ipasavyo.
Msajili wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta akiwasilisha mada mbele ya Wahe. Majaji Wafawidhi
(hawapo pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...