Jiji la Mwanza limepima viwanja 24,000. Ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kuondokana
na Makazi Holela katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Akizungumzia mafanikio hayo hivi karibuni; Mratibu wa masuala ya Urasimishaji, jijini
Mwanza, ambaye ni Afisa Mipango Miji; Athuman. S. Simba alisema; “Katika
kufanikisha utekelezaji uliofanyika; Halmashauri ya Jiji iliunda vikosi kazi vipatavyo kumi
na tatu (13) na kuvipangia majukumu mbalimbali. Vikosi kazi hivyo vilifanya kazi za
uandaaji wa michoro ya mipangomiji, upimaji, ukaguzi wa viwanja na kumilikisha”
Aidha, Katika zoezi zima la upimaji wa viwanja 24,000. Taarifa yake Kaimu Mkurugenzi
wa Jiji la Mwanza; Hosiana B. Kusiga; imesema kuwa; Viwanja 19417 vimepimwa
(Approved), maeneo ya Kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele,
Mahina, Isamilo, na Nyegezi.
Vile vile, Viwanja 5515 vimefanyiwa upimaji wa awali (Dermation).
Kazi ya upimaji
inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Mkolani, Lwahnima, Igoma, Mhandu, Kishiri
na Luchelele. Ambapo Idadi ya viwanja vilivyokamilika na vilivyo kwenye upimaji wa
awali (demarcation) jumla yake ni 25,032.
Utekelezaji wa upimaji huu ni kutoka kwa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi. Mhe. William Lukuvi, kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
kuandaa Hati Miliki za viwanja 35,000 kupitia mradi wa urasimishaji makazi holela .
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la
Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo Ukuta
unaoonekana pichani unategemewa kuondolewa kupisha utengenezwaji
wa barabara za Mitaa.
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la
Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo beckon
zimekuwa zikiwekwa katika viwanja.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipuli, Kata ya Mahina; Rajabu
Jumanne (mwenye shati la bluu) akishuhudia zoezi la upimaji
linavyoendelea katika Mtaa wake, likiongozwa na Mratibu/ Mpima; Yohana
Cleophace wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Muonekano wa Barabara iliyochongwa rasmi na Wataalam
wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na
zoezi la Urasimishaji katika kata ya Ipuli, Mahina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...