Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia umetoa msaada wa vitabu vya ziada 285 kwa wanafunzi 200 wa Shule ya Sekondari Bugisha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za mgodi huo kusaidia maendeleo ya elimu nchini.Msaada huo ni sehemu ya ufadhili ndani ya programu ya CanEducate inayoendeshwa na kampuni hiyo.

CanEducate ilianzishwa mwaka 2010 lengo kuu likiwa ni kudhamini wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika familia maskini. Chini ya programu hiyo, wafanyakazi huchangisha fedha chini ya mfuko maalumu na kisha kampuni ya Acacia hutoa kiwango sawa na kile kilichochangishwa. Fedha hutumika kulipa ada za shule, kununua sare, vitabu na vifaa vya shule kwa wanafunzi.

Wakati wa kuanzishwa kwake, mpango huo uliwasaidia wanafunzi 158 walio karibu na Mgodi wa Dhahabu ya Bulyanhulu. Hata hivyo, kutokana muitikio mkubwa kutoka kwa wafanyakazi na makandarasi wa Acacia, programu imeweza kukua zaidi na kuwafikia zaidi ya wanafunzi 800 kutoka shule zinazoizunguka Buzwagi.

Moja ya sababu ambazo zinachangia kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita, ni ukosefu wa vitabu mashuleni, na gharama za vitabu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kifedha wa wazazi na walezi.
Katika eneo la Buzwagi, mpango huo unahusisha shule tatu za sekondari; Shule ya Sekondari ya Bugisha, Shule ya Sekondari ya Mwendakulima, na Shule ya Sekondari ya Nyasubi ambazo zimetoa wanafunzi bora katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita.

Msaada uliotolewa kwa Shule ya Sekondari ya Bugisha ulisimamiwa na maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa Buzwagi, Yunia Wangoya na Antonia Kiondo.

Msaada huo ulitolewa mbele ya walimu, wazazi na wanafunzi ambao kwa pamoja walitoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya Acacia kwa kuwezesha upatikanaji wa msaada huo mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...