WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na
mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.
“Kama
huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu
ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si
vinginevyo.”
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Septemba 17, 2017), wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.
Amesema
kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao
Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa
hiyo na kulima.
Amesema
ni vema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni
mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie
taratibu zilizopo.Waziri Mkuu amesema Bodi ya Korosho inatakiwa
kuhakikisha inaimarisha zao hilo na kuishauri vizuri Serikali kuhusu namna bora ya kuliendeleza.
Amesema
Serikali inaamini kuwa iwapo kila mdau wa zao la korosho atatimiza
wajibu wake kikamilifu katika kuliendeleza zao hilo kila upande
utanufaika kikamilifu.Hivyo, ni vizuri kila mdau ajitathmini kama
anatimiza wajibu wake kikamilifu, huku akiwaagizaviongozi wa Ushirika waendeshe Ushirika kwa uadilifu mkubwa.
Waziri
Mkuu amesema Serikali haitakuwa tayari kusikia mkulima yeyote
akilalamika kuhusu malipo iwe kwa kupunjwa, kuchelewa ama kutolipwa.
Amesema
katika msimu huu wa biashara ya korosho Serikali haitarajii kusikia
mambo ambayo yalikwaza ufanisi katika misimu iliyopita kama wakulima
kukatwa unyaufu kwa namna yoyote.
“Sheria
ya unyaufu ni miezi sita kutoka korosho inapoanza kuvunwa hadi kuuzwa
na korosho haifiki miezi sita, hivyo wakulima hawahusiki unyaufu kwa
namna yoyote ile na tusisikie tena.”Amesema hali hiyo ikitokea
hawatasita kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. “Nawaagiza viongozi wa
ngazi zote kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa jambo hili.”
Pia
amepiga marufuku Bodi ya Maghala kutoza ushuru wa kuhifadhi mazao kwani
hilo si jukumu lao bali ni la mpangaji wa ghala na wao washughulikie
utoaji wa leseni tu.Katika hatua nyingine Waziri
Mkuu amewataka wamiliki wa maghala ya kuhifadhia korosho kutowazuia
Viongozi wa Serikali kuyakagua kabla na wakati wa biashara.
Amesema
viongozi hao wanatakiwa wasizuiwe kuyakagua maghala hayo hata baada ya
minada ili kujiridhisha na mwenendo sahihi wa uhifadhi wa mazao.Pia
ameagiza kukamatwa na kutaifishwa kwa korosho zote zitakazonunuliwa kwa
njia ya kangomba. Korosho zitaendelea kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi
gharani.
Awali,
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage amesema
korosho ya Tanzania inaongoza kwa ubora duniani, hivyo wazalishaji
wahakikisha sifa na ubora wa zao hilo katika soko la dunia
haushuki.Amesema Serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani
na nje kuwekeza katika viwanda vya kubangulia korosho ili kuiongezea
thamani kabla ya kuisafirisha nje ya nchi.
Mkutano
huo umehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles
Tizeba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage, Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Bw.
January Makamba.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Korosho Bi. Anna Abdallah, Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho,
Wakuu wa mikoa na wilaya zinayolima korosho, Wabunge wanaotoka katika
mikoa inayolima korosho, wanunuzi, wasafirishaji na wenye viwanda vya
ubanguaji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, SEPTEMBA 17, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wadau mahususi wa korosho katika hotel ya Tanga Beach mjini Tanga unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dkt Charles Tizeba akizungumza katika mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Octoba 1 mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Hassani Jarufu akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Mama Anna Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo leo.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...