Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akitoa maelezo kuhusu matumizi ya silaha za jadi hapa nchini na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia uzagaaji wa silaha hizo.
Wzairi wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi katika Wilaya ya Ngara wanapata huduma za maji.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia injinia Stella Manyanya akitoa ufafanuzi kuhusu jinsi Serikali ilivyofanikiwa katika mpango wa elimu bure hapa nchini.
Naibu Waziri
wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole Nasha akizungumzia mkakati wa Serikali
kuhakikisha kuwa Maafisa ugani katika maeneo yote hapa nchini wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika
kuwahudumia wananchi.(Picha
na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...