Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda
wakibadilishana hati baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Kaimu Afisa
Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela.
Zaidi ya wanachama 100 watanufaika na Ushirikiano baina ya Benki ya NMB na Umoja wa Vicoba Tanzania (VIGUTA), baada ya kutiliana saini ya mkataba wa ushirikiano.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo wa ushirikiano jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alisema leo ni siku ya kipee kwa benki hiyo kwa kusaini mkabata wa ushirikiano na Viguta ambao utafungua ukurasa mpya katika sekta ya kifedha nchini.
Alisema benki hiyo siku zote imekuwa karibu na wananchi katika utoaji wa huduma zake na katika ushirikiano huo itatoa mafunzo ya utunzaji wa fedha kwa wateja wao.
Alisema huduma watakayoweza kunufaika nayo wanachama ni ile ya akaunti ya pamoja kupitia vikundi ambapo wanachama wao wataweza kukopa mikopo yenye riba nafuu na kuweza kujua mambo mbalimbali kama kujua salio kwa kutumia simu zao za mkononi.
Alisema benki hiyo imejipanga vizuri kutoa huduma kwa wateja wao pamoja na kutoa elimu kwa kila mtu na ushirikiano huo utakuwa ni endelevu.
Alisema wanaounda akaunti ya pamoja ni makundi ya watu kutoka katika familia, makundi ya wanawake, marafiki na makundi ya whatsApp.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda alisema umoja huo una wanachama milioni 7 huku ukiwa na vikundi 92,000 ambao wananufaika na benki hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...