Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (wa tatu kushoto, mstari wa mbele ) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka hiyo, Imani Nkuwi (kushoto kweke) na viongozi pamoja wafanyakazi wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha. Lengo la ziara hiyo ilikua kuona na kukagua shughuli zinazofanywa na kikosi hicho kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (katikati) akisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa watumishi wa KDU alipotembelea ofisi zao hivi karibuni. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka hiyo, Imani Nkuwi (kulia) na Mkuu wa Kikosi hicho Kanda ya Kaskazini, Ndugu Mkeni (kushoto).
Askari wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Dkt. James Wakibara wakati akitoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi wa kikosi hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...