SERIKALI inatekeleza  Programu ya miaka mitano ya Maendeleo ya Sekta ya Maji nchini (2016/21) ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikoa ya  Mikoa kutoka asilimia 86 hadi 95.

Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaonesha kuwa Idadi ya wateja waliounganishiwa huduma hiyo imeongezeka kutoka 405,095 mwezi Machi 2016, hadi wateja 432,772 mwezi Machi, 2017 ambapo asilimia 97 ya wateja hao wamefungiwa dira za maji ili kulipia huduma ya maji kulingana na matumizi. 

Pamoja na ongezeko hilo la uzalishaji wa maji bado mahitaji ya maji ni makubwa katika maeneo ya Miji Mikuu ya Mikoa ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, hatua iliyoilazimu Serikali kuwekeza katika miundombinu ya maji na kuzijengea uwezo mamlaka za maji ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika Jiji hilo.

idadi ya maunganisho kwenye mtandao wa majisafi ya Jiji la Dar es Salaam imeongezeka kutoka wateja 155,000 mwezi Machi, 2016 hadi kufikia wateja 182,721 mwezi Machi, 2017, kutokana na kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji kutoka Tsh. Bilioni 7.1 Machi, 2016 hadi Tsh. Bilioni 8.3 Machi, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jiji la Dar lina wakazi takriban milioni tano lakini cha kushangaza ninyi mnawateja wasiozidi laki mbili. Hii inaonyesha kwamba maji yenu hayawafikii wananchi ipasavyo. Msipo sambaza haya maji kwa wananchi DAWASA itapata hasara na mwishoe kufa kabisa. Ikifika 2020 lazima muwe na wateja wasiopungua milioni kwa DSM only otherwise you r going to FAIL DSM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...