Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta leo ameongoza waombolezaji katika mazishi ya watoto watatu waliofariki dunia kwa mlipuko wa bomu kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Marehemu hao - Johnson Daniel, Lendisi Saitabau na Samweli Nyangusi -walifariki dunia Ijumaa iliyopita katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale walipokuwa wakichunga ng'ombe. Inasemekana walilipukiwa na bomu walipokuwa wakilichezea wakidhani ni mpira.
Mazishi hayo yamefanyika katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nafcon wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya wanafunzi wenzao mara baada ya kuwasili nyumbani kutokea hospitali ya wilaya ya Monduli kabla ya mazishi katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta akitoa rambirambi za serikali kwenye mazishi hayo katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.
Ibada ya mazishi katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha
Sehemu ya waombolezaji kwenye mazishi hayo
Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya majeneza ya marehemu hao wakielekea makaburini kwa mazishi. Picha zote na HD TEAM MEDIA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...