Violet
Brown aliyezaliwa tarehe 10 March 1900 na kufariki dunia jana Ijumaa tarehe 15 September 2017 ni
mwanamke wa Jamaica ambaye hadi mauti yanamkuta ndiye aliyethibitishwa kuwa mtu
mwenye umri mkubwa kuliko watu wote duniani kufuatia kifo cha aliyekuwa
anashika rekodi hi mwanamama wa Italia Emma Morano aliyezaliwa tarehe 29 November 1899 na kufa tarehe 15 April 2017 akiwa na umri wa miaka 117 na siku 189.
Mama
Violet pamoja na Nabi Tajima (pichani kulia) wa Japan (aliyezaliwa tarehe 4 August 1900) walikuwa
watu wawili wa mwisho duniani waliojulikana kuwa walizaliwa katika karne ya 19.
Hivyo rekodi hiyo ya uhai mrefu inashikiliwa sasa na Mama Tajima.
Akiwa
mmoja wa watoto wane wa mzee John Mosse, mchemsha sukari katika kiwanda kwenye
shamba la miwa, na mama Elizabeth Riley,
Mama Violet aliolewa na Bw. Augustus Gaynor Brown na wakajaaliwa kupata jumla
ya watoto sita, wane wao wakiwa hai
wakati wa kifo chake jana.
Kwenye
Mahojiano Mama Violet alisema yeye alikuwa na afya bora kuliko wanawe na hakuwa
na maradhi yoyote. Alipoulizwa siri ya uhai wake mrefu alisema hakuna siri kwa
kweli.
“Haki
ya nani tena ni kweli watu wakiniuliza nakula nini na kunywa nini, nawaambia
nakula kila kitu isipokuwa kitomoto na kuku. Pia sinywi pombe na y ale mambo Fulani (ganja) situmii…”alisema
Mama Violet.
parent.[15] Death Brown died on 15 September
2017 at a hospital in Montego Bay, Saint James Parish, of heart failure
complicated by dehydration at the age of 117.[16]
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...