Na Richard Mwaikenda,Lindi 
 JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike. 
 Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana. 
" Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. 
 "Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga
Amewataka waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike. Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni. 

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. 
 Timu ya soka ya wanawake mkoani Lindi wakitambulishwa katika hafla hiyo. Nao wanatarajia kujiunga na Girl Guides
 Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
 Girl Guides wapya wakila kiapo
 RPC Mzinga akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...