MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamiria kurudi katika familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaitwa 'Kipotabo'Septemba 19 mwaka huu ambayo imetengenezwa katika studio za Combination Sound chini ya mtayarishaji Man Water na video kutengenezwa na Kwetu Studio.
Akizungumzia ujio wake mpya Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz' alisema kuwa amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri na kwa sasa kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.
Ne-mo ujio wake utakuwa wa aina yake na Watanzania hawatajutia kumsubiri Ne-Mo arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya wake umetokana na masomo ambapo aliamua kutulia amalizie masomi kisha aendelee na Harakati za Muziki na alikuwa masomoni akiwa amesomea masuala ya 'Mass Communication' na anaeleza kuwa sasa ametulia na amepata 'Mameneja ' ambao wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo katika muziki.
"Nimejipanga vuzri pamoja na mameneja wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba mashabiki wa muziki Tanzania wanipokeekwa mara nyinyingine, nilitoka kidogo kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi katika muziki"alisema Ne-mo.
Alisema kwa upande wa mtindo wa Rap na Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa Hip Hop mtaani na kukubalika na kila kundi la jamii., miaka michache iliyopita waliibukakina Child Benz na Nako 2 Nako ambao walisaidia kujenga misingi ya kuufanya muziki wa Hip Hop kukubalika kibiashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...