Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat gwajima na wenzake watatu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha maahtaka dhidi yao.
Mbali na Gwajima, washtakiwa wengine walioachiwa huru ni Askofu msaidizi Yekonia Bihagaze (39) mkazi wa Kimara Stop Over, George Mzavaa (43) anaishi Ilala mabHeofrey Milulu (31) mchungaji mkazi Wa Kumara Baruti.
Askofu Gwajima alikuwa akikabiliwa na shtaka la kushindwa kutunza mahali pa usalama bastora na risasi wakati wenzake wakikabikiwa na tuhuma za kukutwa na bastola hiyo pamoja na risasi 20
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ambaye amesema upande Wa mashtaka kupitia mashahidi wake wameshindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo.
alisema kuwa kesi hiyo haijathibitika kwa viwango vinavyotakiwa na kwamba begi lililokuwa na bunduki na risasi virudishwe kwa Askofu Gwajima.
Alisema kuwa hakuna uthibitisho kwamba Gwajima alizembea kusalimisha silaha hizo Polisi na pia hakuna ubishani kwamba alikubali kuripoti katika Ofisi ya Mpelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) ambapo alifika akiwa na begi hilo lenye bunduki na risasi 20.
Ameongeza kuwa hakuna ushahidi kama mshitakiwa hakukaguliwa na polisi yeyote hadi alipokutana na ZCO na kwamba wakati anahojiwa alipoteza fahamu akiwa na begi lake hadi alipozinduka akiwa Hospitali ya TMJ,
Hakimu Mkeha ameongeza kuwa, uteetezi uliotolewa unaonyesha wazi mshitakiwa huyo alikuwa makini nyakati zote akiwa na silaha zake kwani hata alipokuwa kitandani alililinda.
"Ingawa sheria kwa namna yoyote haielezi ni lazima shahidi fulani aje lakini kwa mazingira yaliyokuwepo hospitali ambayo kulikuwa na walinzi hawa wangeweza kuletwa kama mashahidi wa upande wa mashitaka lakini hawakuletwa na hawakuingizwa kama wazembe katika kesi hii kitendo ambacho kinaongeza shaka kwa upande wa mashitaka,
Ameongeza kuwa kutokana na mashaka hayo, hakuweza kupata sababu za msingi za kutoamini ushahidi wa nesi ambae alikuwa ni shahidi wa utetezi aliyeeleza namna mambo yote yalivyotokea.
"Nimelazimika kuwaachia huru washtakiwa wote kwani upande wa mashtaka hawajaweza kuthibitisha kesi kwa kiwango kilichotakiwa" amesema Mkeha
Katika hati ya mashtaka ilidaiwa, kati ya Machi 27 na 29, mwaka 2015 jijini Dar ea Salaam, Gwajima akiwa mmiliki na aliyesajiliwa kutunza bastola aina ya berreta yenye namba za usajili CAT 5802 pamoja na risasi zake tatu na risasi 17 za bastola aina yabshortgun alishindwa kuitunza silaha hiyo na kuiacha mikononi mwa Bihagaze, Mzava na Milulu ambao hawatambuliki kisheria.
Aidha washtakiwa hao wakiwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni walikutwa na silaha pamoja na risasi hizo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...