Mkutano huo uliokutanisha viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa 27 nchini unafanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo ambao utafanyika kwa muda wa siku mbili (Septemba 15 na 16,2017),Shigela alisema serikali inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii.
“Ukitaka maendeleo katika jamii lazima ushirikiane na vyombo vya habari,na hata tunapoelekea katika Tanzania ya viwanda ni vyema vyombo vya habari vihusike”,alieleza. Alitumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili katika kazi yao ya uandishi wa habari huku akiwaasa kujiendeleza kielimu ili kufanya vizuri zaidi katika kazi yao.
“Vyombo vya habari vinafundisha,vinaelimisha,vinahamasisha ,vinakosoa na kufichua maovu na ili kutimiza haya ni vyema mkazingatia maadili yenu,mfanye kazi kwa usawa bila upendeleo lakini pia ni vyema mkawa wazalendo”,aliongeza. Kwa Upande wake rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili tasnia ya habari ni uwepo wa sera na sheria zinazobinya uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Habari ya habari ambayo baadhi ya vifungu vyake siyo rafiki kwa waandishi wa habari. “Tunaiomba serikali ifanye marekebisho katika baadhi ya vifungu kwenye sheria hii ambavyo siyo rafiki kwa vyombo vya habari”,aliongeza Nsokolo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...