Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na sekta wa usafiri wa anga wameandaa kongamano usafiri huo kwa lengo kujadili namna ya kuinua na koboresha zaidi sekta ya usafiri wa anga katika uchumi wa taifa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kutokana na sekta ya Usafiri wa Anga katika kufikia uchumi wa kati 2025.
Amesema kuwa katika mada watakazo jadili ni kupungua kwa shehena zinazosafiri kupitia viwanja vya ndege ikiwemo Samaki zinazovuliwa katika Ziwa Vicktoria kutumia kiwanja cha ndege cha Entebe cha nchini Uganda na Maua ya Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha kutumia uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya.Hamza amesema mkutano huo ndio utatadhimini hali ya usafiri ili kuboresha masuala mbalimbali ya usafiri wa anga katika kufanya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kiunganisha kwa safari za ndege.
Amesema kuwa mkutano huo unafanyika mara mbili kwa mwaka ili kuangalia masuala mbalimbali ya usafiri wa anga kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi.Mgeni Rasmi katika Mkutano huo atakuwa ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi- Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho.
Amesema katika ukaguzi wa Shirika la Usafiri wa Anga (ICAO) kwa Mamlaka hiyo imepata asilimia 64.4 katika mwaka huu kutoka asilimia 37. 5 mwaka 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya mkutano wa wadau wa usafiri anga utaofanyika Septemba 18 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Wandishi wa habari wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari wakati akitangaza mkutano wa wadau utaoanza kesho, jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...