Rais wa TCIA akifafanua jambo mbele wa wafabiashara walioshirika katika mkutano mkuu wa mwaka.Chama cha wafanyakazi, kilimo na viwanda Tanzania kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka pamoja na kuzindua mfumo mpya wa ulipiaji bidhaa kwa njia ya mtandao ‘LIPA FASTA’ lengo kubwa likiwa ni kusaidia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi. Mfanyabiashara na mwanachama wa TCCIA ndugu mustafa hassanal akisalimiana na mgeni rasmi ndugu Raymond Mbilinyi katika mkutano mkuu wa mwaka, pembeni ni makamu Rais wa TCCIA ndugu Octavian Mshiu

Huduma hii imezinduliwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa TCCIA ambapo wanachama wote wa TCCIA pamoja na wafanyabiashara mbalimbali walihudhuria mkutano huo kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa huduma hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda akiongea na wafanyabishara waliohudhuria katika mkutano mkuu wa mwaka

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurungezi Mtendaji ndugu Gotrid Muganda alisema ‘LIPA FASTA ni mkombozi kwa wafanyabiashara wote katika kurahisisha njia zao za kufanya malipo. Kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi, sasa hawana haja ya kuwa na wasiwasi katika kufanya malipo kwani mfanyabiashara anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake.Mfumo huu utasaidia wafanyabiashara kupata cheti cha uwasili kwa muda mfupi.Rais wa TCCIA ndugu John Mayanja akifafanua jambo katika mkutano hu0
Nae makamu wa Rais wa chama Ndugu Octavian Mshiu amesema’ mpango huo utaendeshwa na TCCIA kuanzia ngazi ya wilaya ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao nje ya nchi’
LIPA FASTA ni zaidi ya njia ya malipo kwani hapa hata watanzania waishio nchi za nje ya nchi watapata nafasi ya kupata taarifa sahihi za soko, kuhifadhi taarifa sahihi za soko na bidhaa zilizopelekwa kwenye maitaifa mbalimbali pamoja na kumwezesha mfanyabiashara kufanya malipo popote alipo.Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wakifwatila mkutano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...