Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi katika Wilaya ya Arumeru Kata ya Makiba kijiji cha Valeska mkoani Arusha; wameonyesha kuelewa umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa kiasi cha kujiwekea mkakati wa kuhakikisha nishati ya umeme muda wote inakuwepo ili zoezi la Usajili linaloendelea kutosimama.
Pengine hii ni tofauti na mazoea ya siku zote katika uendeshaji wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa maeneo ambayo zoezi kama hilo limewahi kufanyika kiasi cha kuamsha morali zaidi kwa watumishi kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi kushiriki zoezi hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo; mtendaji wa Kata hiyo amesema wao kama Kata wamehamasisha wananchi kujitokeza kusajiliwa na kutokana na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi wana imani Kata yao watakamilisha zoezi la Usajili ndani ya muda uliopangwa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akikagua fomu ya Bwana Kitomari baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya usajili Vitambulisho vya Taifa kabla ya kwenda kwenye hatua ya upigaji picha. Hapa ni Kata ya Makiba kituo cha CCM Arumeru Arusha ambako zoezi hilo linafanyika.
Hawa ni Watendaji katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Valeska wakiendelea na zoezi la kuwahakiki wananchi wao na kuwathibitisha kuwa ni wakazi halali wa eneo lao kabla ya kuwaidhinisha kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani Arumeru.
Huu ni muonekano wa nje ya jengo ambako usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaendelea Kata yaMakiba kijiji cha Valeska. Baadhi ya wananchi wakiwa wanabadilishana mawazo huku wakisubiri kupatiwa huduma.
Afisa Usajili Wilaya ya Arumeru ndugu Edward Bujune akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la kuwasajili wananchi wa Wilaya ya Arumeru likiendelea.
Meneja Mifumo ya Komputa ndugu Mohamed Mashaka akirekebisha moja ya Kamera ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la Usajili Wilayani Arumeru.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...