Na Teresia Mhagama, Tabora
Imeelezwa kuwa miamba iliyo katika Bonde la Eyasi Wembere hususan mabonde madogo (sub basin) ya Wembere na Manonga yaliyopo katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Singida na Simiyu inawezekana kuwa na mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia.
Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo katika Mkutano na Wananchi uliofanyika katika kijiji cha Mwashiku wilayani Igunga mkoani Tabora. Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry.
Viongozi hao walitoa kauli hiyo baada ya timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania kufanya ziara katika Bonde hilo hususan mabonde madogo ya Wembere na Manonga na kutembelea miamba inayoonekana katika maeneo ya Sekenke mkoani Singida, na vijiji vya Mwanzugi na Kining'inila mkoani Tabora.
Sehemu ya Bonde la Manonga mkoani Tabora ambalo miamba yake inaonesha uwezekano wa kuwa na viashiria vya Mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia.
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika miamba inayoonekana katika kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga ikiwa ni ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika.
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika Bonde la Manonga lililopo katika kijiji cha Kining’inila mkoani Tabora ambapo pia walichukua sampuli za miamba katika Bonde hilo ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika eneo la Sekenke mkoani Singida ambapo miamba ya Bonde la Wembere inaonekana ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere. Wa Tano kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande, wa Pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...