Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amekabidhi Vitambulisho vya Matibabu ya Bure kwa wazee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.
Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1,080 watapata Vitambulisho huku wazee 540 ndio wamekabidhiwa leo hii na wengine wataendelea kupokea kutoka katika Ofisi ya Mbunge kwa muda wa wiki nzima huku matarajio yakiwa ni kuwafikia wazee 3,284 katika jimbo zima.
Aidha, sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi.
Mhe. Ngupula amepongeza jitihada za Mheshimiwa Bashe katika shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mhe. Bashe alipohojiwa alisema ya kuwa ..."wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu ni jukumu letu sasa kama vijana na taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia Matibabu bora na kuwaondolea gharama za Matibabu ili kuleta unafuu wa maisha"
"Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za Vitambulisho ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini anapata kitambulisho cha matibabu ya Bure".... Hussein Bashe.
Jimbo la Nzega Mjini ni jimbo pekee ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega hivyo tukio hili linaifanya Halmashauri hii kuwa moja kati ya Halmashauri chache kitaifa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...