Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe amekagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla. 
 Mafanikio ya ujenzi wa shule hii ni maono ya Mheshimiwa Bashe katika kuhakikisha watoto wa masikini wanapata elimu ili kuweza kujikwamua na umasikini. 
 Mhe. Bashe amesema kuwa  anaamini ya kuwa ..."Elimu ndio njia pekee ya kumkomboa mtoto wa masikini" 
 Aidha Shule hii itakua na uwezo wa kupokea wanafunzi kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Sita huku msisitizo ukiwa ni masomo ya Sayansi. Ujenzi wa shule hii unaendana na ujenzi wa kituo cha Afya ambacho kitahudumia wananchi pamoja na wanafunzi ambao watakua wanasoma katika shule hiyo. 
 Bashe anasema "Tuna vipaumbele vingi lakini kile cha kwanza na msingi kwetu ni Elimu ya watoto wetu" "Hivyo nitahakikisha ninaboresha miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini na kama sehemu ya urithi kwa watoto wa masikini".
 Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega ukiendelea
 Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akikagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
  Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akiongea baada ya kukagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akiongea baada ya kukagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...