Na Ramadhani Ali – Maelezo .
Wagonjwa wanaotumia dawa aina ya Methadone kama tiba baada ya kuathirika kutokana na dawa za kulevya na wanaoutumia aina nyengine ya dawa kwa njia za siri wamepatiwa muarubaini baada ya kupatikana vifaa maalumu vya kumgundua mtumiaji kwa kumpima mkojo.
Vifaa hivyo vinavyojulikana kwa jina la DOAKIT vimetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu (UNODC).Mratibu wa Mradi wa Taifa wa kupambana na HIV/AIDS kwa wafungwa, Immaculate Nyoni ambae ni afisa wa UNODC Tanzania amemkabidhi vifaa hivyo Mratibu wa huduma za ukimwi kwa watu wa makundi maalum Zanzibar Dkt. Shaaban Hassan katika hafla iliyofanyika Kliniki ya Methadone iliopo ndani ya hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- chekundu.
Immaculate alisema UNODC itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia tiba sahihi wagonjwa walioathirika na dawa za kulevya.Alisema kwa kuanzia wameleta DOAKIT 1500 ambazo zinaweza kutumika kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mujibu wa idadi ya wagonjwa wanaotumia Methadone waliosajiliwa katika kliniki hiyo.
Daktari dhamana wa hospitali ya Kidogochekundu Dkt. Khamis Othman alilishukuru shirika la UNODC kwa kuwapatia msaada huo ambao kwa kipindi cha mwaka mmoja walikuwa na upungufu mkubwa na kupelekea baadhi ya wagonjwa kutumia aina nyengine ya dawa bila kujulikana.
Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Bi. Immaculate Nyoni akimkabidhi boksi lenye vifaa vya kupimia mkojo watumiaji dawa ya Methadon ambao wanatumia aina nyengine ya dawa kinyume na taratibu katika hafla iliyofanyika Kliniki Methadone Kidongochekundu.
Rais wa watumiaji dawa ya Methadon Zanzibar Hilal Nassor akizungumza na wandishi wa habari baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuwatambua watumiaji wa tiba ya Methadone na baadae kutumia dawa aina nyengine.
Baadhi ya watumiaji dawa za Methadone wakisubiri kupatiwa huduma katika Kliniki yao iliyopo Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- Chekundu Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...