Na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari Polisi kote nchini kushiriki michezo ili kujenga Afya,ukakamavu na urafiki baina ya wenyewe kwa wenyewe na raia.
IGP Sirro ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji wa TAEKWONDO waliofanya vizuri katika michezo ya Taekwondo Pumsae (kucheza Kata), Taekwondo Gyeokpa ( kuvunja kibao kwa kuruka Juu) na Taekwondo Gyeorugi (Mapigano) iliyomalizika hivi karibuni ambapo timu ya Polisi iliibuka na ushindi wa kwanza katika timu 17 zilizoshiriki.
Sirro alisema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo michezo ya aina mbalimbali na atahakikisha Askari na Maofisa wanapata fursa ya kushiriki michezo kwakuwa kwakufanya hivyo kutasaidia pia kulitangaza Jeshi la Polisi na kujenga mahusiano na jamii.
"Hakikisheni hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji bali tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana kwa kuwa ari na morali ipo"Alisema Sirro.
"Hakikisheni hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji bali tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana kwa kuwa ari na morali ipo"Alisema Sirro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi Sambamba na Askari Polisi walioshiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya mchezo wa Taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na askari wa jeshi hilo wanaounda timu ya Taekwondo ambao walishiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya Taekwondo yaliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association) yaliyoshirikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simoni Sirro akimvisha medali askari Polisi ambaye ni miongoni mwa askari waliojinyakulia medali katika mashindano taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association). Picha zote na Jeshi la Polisi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...