Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza
alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa
na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo
kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini
na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga
(kulia) akikagua baadhi ya vifungashio vya asali alipotembelea shamba la miti
Sao Hill kwa ajili ya kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo
mkoani Iringa hivi karibuni. Asali inayozalishwa na shamba hilo imefanyiwa
vipimo nchini Ujerumani na kugundulika kuwa ni bidhaa bora isiyo na viambata
vya kemikali ya aina yeyote. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza
na Afisa Ufugaji Nyuki wa shamba hilo, Said Abubakar.
Meneja wa shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kushoto) akimueleza Mhe. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
(kulia) kuhusu moto uliovamia hekta 77 za shamba hilo na hatua
zilizochukuliwa kuudhibiti alipotembelea
kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa
hivi karibuni, alisema moto huo uliozuka hivi karibuni ulianzia kwenye mashamba
ya wananchi haukuwa na madhara makubwa.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga kuhusu utafiti unaofanywa na shamba hilo kwa kushirikiana na Kampuni ya Art
International kuhusu uvunaji wa utomvu kwa ajili ya kutengeneza madawa
mbalimbali, bazooka (chewing gums) na ‘gel’ kwa ajili ya kujiongezea kipato
alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi karibuni. Kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mhe. Jamhuri David.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani)
kuhusu njia mpya ya kuzalisha mbegu za miti kwa njia ya vikonyo ili kuongeza
zaidi uzalishaji alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi
karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili
kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa
viwanda.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...