Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema jana kuwa katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya atagawa nyumba 18 zilizojengwa na wanachama wa mtandao kwa njia ya kuchangiana na atakabidhi alama 55 kwa wanachama.
Alisema katika maadhimisho hayo ambayo SHIWATA huadhimisha siku hiyo kila mwaka kwa matukio mbalimbali mwaka jana walikabidhi fedha kwa watu waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.
Taalib alisema SHIWATA ambayo mpaka sasa imekwisha kabidhi nyumba 268 zilizojengwa kwa njia ya kuchangiana pia imekuwa ikiendesha matamasha ya wasanii mbalimbali kuonesha vipaji vyao.
Alisema Julai mwaka huu SHIWATA iliendesha tamasha la wasanii wote na Desemba mwaka huu kutakuwa na mashindano ya soka ambayo yalianza mwaka jana na timu ya maveterani ya Kitunda iliibuka kuwa mabingwa kati ya timu sita zilizoshindana.
Katika hatua nyingine wanachama wa SHIWATA ambao mashamba yao yanachukuliwa na serikali kwa ajili ya kujenga viwanda wameazimia kutafuta mashamba mengine kando kando ya reli ya Kati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...