Katika kuazimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ameongoza umomoja wa Vijana CCM, Wilaya ya Ilala kufanya usafi na kugawa misaada ya kijamii katika Hospital ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mhe. Mjema amesema , Wameamua kufanya usafi na kugawa zawadi hizo ili kumuenzi Babawa Taifa na amewapongeza vjiana wote walijitokeza katika shuguli hiyo kwani nitendo la uzalendo amabalo linawafanya watu wengi kumkumbuka mwalimu Nyerere kwa uadilifu wake alivyo litumika Taifa enzi ya uhai wake.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospital hiyo Helmani Gonyani, amewashukuru vija wa umoja huo kwa kutembelea hospitali hiyo na kufanya usafi na kuwataka tena iwapo wata pata nafasi siku nyingine wafanye hivo kwani wamefariji wagonjwa na kuhamasisha umoja wa kitaifa.

Mkuuwa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema aliye vaaqkilemba ,aliye upande waq kushoto ni Diwani wa kata ya Ilala Mhe. Saad Kimji akifagia na vijana wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Ilala katika Hospital ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo katika kuelekea madhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Mwalimu JK nyerere.
Mmoja wa viongozi wa umoja wa vijana CCM ilala akimpati zawadi ya Sabuni mama mzazi Ruth Eliya aliye jifungua jana katika Hospital ya mnazimoja ,aliye upande wamisho kulia ni Mkuuwa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...