Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiangalia picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, kabla ya kuzizindua jijini Dar es Salaam jana. Walioshika bango lenye picha za stempu hizo kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akikabidhiwa bango lenye picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake na kaimu postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati wa uzinduzi wa stempu hizo jijini jana. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), na kaimu Postamasta Mkuu Bw.Macrice Mbodo (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Shirika hilo, kwenye ofisi ya Posta uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere mara baada ya kumalizika uzinduzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...