Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 

Rais mstaafu wa awamu ya nne ,dk.Jakaya Kikwete ,ametoa rai kwa wadau na viongozi ambao wametokea katika chimbuko la shule ya sekondari ya Kibaha;” ,Kuangalia namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo inasababisha mlundikano wa wanafunzi madarasani.

Aidha amesema mbegu ya kuwa yeye mwanasiasa ilipandwa shuleni hapo, baada ya kuchaguliwa kiongozi wa baraza la shule kutokana na harakati zake za kutetea haki za wanafunzi .

Dk.Kikwete aliyasema hayo shirika la elimu Kibaha ,wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha ambako alipata elimu yake ya sekondari mwaka 1966 hadi 1969. Alisema ,atashirikiana na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa .

Dk.Kikwete alisema , haipendezi na hajafurahishwa na hali ya miundombinu ilivyokuwa chakavu hali inayoathiri mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji . Rais huyo mstaafu wa awamu ya nne ,alieleza changamoto hizo si sababu ya kushindwa bali uwepo wa changamoto huongeza umakini ,bidii na ubunifu ili kukabiliana nazo .
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk.Jakaya Kikwete ,akitoka kutembelea bweni alikuwa analala wakati akisoma shule ya sekondari Kibaha mwaka 1966-1969, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo,huku akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa pili kushoto,na viongozi wa shule ya sekondari Kibaha na shirika la elimu Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo maalum katika mahafali hayo. 
Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, Mkoani Pwani, wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo .

Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...