Benki ya TPB imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha.

Lengo la kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki yao.Alisema pia wananchi wa Arusha, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

‘Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la benki ya TPB Mto wa Mbu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Profesa Lettice Rutashobya. Uzinduzi wa tawi hilo la Mto wa Mbu ulifanyika jana huko Mto wa Mbu, Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja, Ester Mfuru, wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, wakati wa uzinduzi wa tawi hili. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof. Lettice Rutashobya.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Bank Profesa Lettice Rutashobya, akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililopo Mto wa Mbu Arusha. Akitazama ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya TPB Mhe. Dkt. Philip Mpango (c) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. Kutoka kulia waliokaa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshigi na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Lettice Rutashaobya. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Waliosimama nyuma ni baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...