Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar viongozi watakaochaguliwa kupitia Uchaguzi wa ngazi ya Wilaya ya Kaskazini “B” kichama Unguja kuwa mstari wa mbele kukemea vikali tabia ya makundi na safu za uongozi zenye nia ya kuhatarisha uhai wa CCM katika Wilaya hiyo.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo wa kuwachagua viongozi wa nafasi mbali za ngazi hiyo huko Mahonda katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema matarajio ya CCM ni kuona viongozi wanaochaguliwa katika uchaguzi huo wanachukia kwa vitendo uwepo wa baadhi ya makada wanaoendekeza makundi, Safu na rushwa ndani ya chama hicho.
Dk.Mabodi alieleza kwamba msimamo wa CCM ni kuhakikisha Katiba, kanuni na miongozo inasimamiwa na kufuatwa ipasavyo ili kupata viongozi na makada wenye uwezo wa kuendeleza mafanikio ndani ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Aidha aliwambia viongozi watakaopata nafasi ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi huo wahakikishe wanajenga ngome imara ya kisiasa katika wilaya hiyo sambamba na kuwashawishi wapinzani waliomo katika Wilaya hiyo kujiunga na CCM kwani ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wananchi wote.
-Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.

Baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk. Mabodi huko Mahonda.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano huo Balozi Seif Ali Idd akipiga kura katika uchaguzi wa CCM ngazi ya Wilaya ya Kaskazini "B" uliofanyika leo huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...