Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

“Mimi nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.

 Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
 “Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo. 
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...