Na Mathias Canal, Geita

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kuwafukuza kazi maafisa watatu wa idara ya Maendeleo ya Mazao katika sehemu ya pembejeo ambao wamebainika kuhusika moja kwa moja na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita Mhe Tizeba alisema kuwa kufukuzwa kazi kunajili kutokana na ukosefu wa umakini na usimamizi mzuri wa sheria ya ununuzi wa Umma ikiwemo kusababisha kuchapishwa kwa vocha za pembejeo zenye thamani ya Tshs 78,054,970,000 ambazo ni zaidi ya bajeti halisi iliyotengwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa kiasi cha Tshs 42,587,419,200

Watumishi waliofukuzwa kazi ni Bw Shenal S. Nyoni aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha pembejeo, Aliyekuwa Afisa kilimo Daraja la I Bw Michael G. Mayabu na Bw Franks F. Kamhabwa.

Waziri Tizeba ametumia mamlaka hayo mara baada ya kupitia taarifa ya waraka wa mkakati wa utekelezaji na Usimamizi wa utoaji wa Ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa kutumia vocha wa mwaka 2015/2016 ambapo pamoja na mambo mengine uliainisha utaratibu wa usimamizi wa zoezi la utopaji wa ruzuku ambao ulilenga kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...