Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella lipo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).

Hayo yameelezwa leo Octoba 30 na wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuja kwa ajili ya kutajwa,  

"Mheshimiwa,  jalada  halisi la kesi hii limetoka ofisi ya upelelezi mkoa wa Temeke (RCO) na sasa lipo kwa DCI." Amesema Mwita.

Kufuatia Maelezo hayo,, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, mwaka  huu pia ameusisitiza upande wa Mashtaka wakamilishe mapema upelelezi.

Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka huu, washtakiwa hao  wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada  wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Tukio hilo, linalodaiwa kufanyika Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao, awali  Februari 23, 2016, waliachiwa huru katika kesi ya mauaji namba 32 ya mwaka 2016 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa.

Baada ya kufutwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikifanana na hii walikamatwa  na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...