Harbinder Sethi
Na Dotto Mwaibale

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14.

Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea.

Amri hiyo ya mahakama imetolewa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi ilipangwa leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba shauri lipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, wakili Joseph Makandege anayemwakilisha Sethi alieleza kuwa kumekuwepo mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake akapatiwe matibabu na kufanyiwa uchunguzi Muhimbili.

“Hadi leo asubuhi tuliwasiliana na mteja wetu na kubaini hajapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama amri za Mahakama zilivyoagiza, hivyo ni rai yetu kwamba kitendo hicho cha kutotekelezwa amri za Mahakama ni ukaidi wa amri halali za Mahakama yako tukufu,” amesema Makandege.

Alisema kwa kuwa upande wa mashtaka umekaidi amri za Mahakama, anaomba itoe adhabu inayostahili.Makandege alisema kitendo cha upande wa mashtaka cha kutotekeleza amri za Mahakama kinasigana na kukiuka mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...