Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema utamaduni wa watu wa Zanzibar wa kuheshimu dini zote ni nguzo imara iliyosimamisha  amani na utulivu nchini.
Balozi Seif ameyasema hayo afisini kwake Vuga wakati akipokea msaada wa fedha taslim shilingi milioni 10 kwa ajili ya sekta ya afya kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini.
Amesema tangu zamani waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu wamekuwa wakiishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii bila ya mikwaruzano. 
Amesema msaada huo wa fedha ambao umekusudiwa kwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja umekuja wakati muwafaka ambapo Serikali imo katika mipango ya kuimarisha huduma zote zitolewazo hospitalini hapo.
Akikabidhi msaada huo wa shilingi milioni 10 kwa Makamo wa Pili wa Rais, mchungaji Bariki Urassa amesema madhehebu yao ya Efatha hupeleka misaada yake pale inapohitajika.
Amesema wakati wa ziara ya kiongozi wao Mkuu wa Efatha Duniani mchungaji Josephate Elias Mwingira alipoonana na makamo wa Pili wa Rais aliahidi kuisaidia Hospitali ya Mnazi Mmoja, ahadi ambayo amekuja kuitekeleza kwa niaba yake. 
Sherehe fupi ya makabidhiano ya msaada huo ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah ambaye kwa niaba ya Wizara yake ameahidi kuutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa.
Katibu Mkuu huyo amesema Wizara yake itatoa mashirikiano ya karibu kwa wale wote wanaotaka kuchangia na kutoa wito kwa taasisi nyengine  za  ndani na nje kujitokeza kutoa misaada yao kwa Wizara yake ambayo imepewa majukumu makubwa ya kuwahudumia kifya wananchi wote wa Zanzibar. 
 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akipokea msaada wa fedha taslim shillingi milioni 10 kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha kwa ajili ya hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akionesha msaada huo wa fedha taslimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. WANA WA MUNGU HUO NDIYO UPENDO WA WANA WA EFATHA KWA KUONYESHA KWA MATENDO KUWA MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO. ASANTE MUNGU KWA MTUMISHI WAKO MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA AMBAYE ANAJITOA KUHAKIKISHA YALE ANAYOTUFUNDISHA TUNAYAISHI. AMEN
    MWANA EPHATA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...