NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Mtwara.

WAHANDISI na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wanapambana usiku na mchana kuzifanyia matengenezo mashine za kufua umeme, ili kuondoa tatizo la kukosekana kwa umeme kwa vipindi virefu kila siku kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.

 Akizungumza mjini hapa leo Oktoba 14, 2017, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia Uzalishaji, Mhandisi Kaitwa Bashaija, (pichani juu), amesema kwa sasa Wahandisi na mafundi wa shirika hilo wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kutengeneza mitambo hiyo na hivyo kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

K-VIS BLOG ilishuhudia mafundi hao wakifanyakazi ya kurekebisha mitambo hiyo katika kituo cha kuzalisha umeme wa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara leo Oktoba 14, 2017.

“Mitambo hii ina kiasi cha mika 10 tangu ifungwe, na kadiri miaka inavyokweda ndivyo ongezeko la uhitaji wa umeme hususan mkoani Mtwara linazidi kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi,” Alisema Mhandisi Bashaija.

Alisema, miaka michache iliyopita baadhi ya mitambo iliweza kuzimwa na bado hali ya umeme ilikuwa imara.Wiki iliyopita Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliagiza TANESCO kufanya juhudi za ziada kuhakikisha tatizo la umeme mkoani Mtwara na Lindi linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017
 Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017
 Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka. Kulia ni Mhandisi Bashaija.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...