Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
WASICHANA walioko shuleni wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.
Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.
Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400 kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .
Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...