Kesi ya kutumia lugha chafu ya Matusi dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli inayomkabili mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee kuanza kusikilizwa Nivemba 8, huu.
Hatua hiyo inakuja baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Janeth Magoho kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika na kumsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali (PH).
Kabla ya kusomewa PH, Halima alikumbushwa shtaka hilo linalomkabili, kuwa alitenda kosa Julai 3 mwaka huu, katika Makao Makuu ya Chadema Kinondoni.
Anadaiwa kumtusi Rais kiwa "anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Akisomewa PH, Halima amekubali maelezo yake binafsi likiwamo jina lake, anaishi Makongo, yeye ni Mbunge na Siku ya tukio ya Julai 3,2017 alikuwa katika fisi ya Chadema.
Aidha, amekanusha kumtukana Rais wa Januhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.Akiendelea kusomewa PH na wakili Magoha mshtakiwa Halima alikubali kuwa Julai 4, mwaka huu alikamatwa katika eneo la Kibangu wilaya Kinondoni na kupelekwa kwa katika ofisi ya ZCO kwa mahojiano.
Hata hivyo, Halima alikana maelezo ya kuwa wakati akihojiwa alikubali kuwa alitoa lungha ya matusi dhidi ya Raid Magufuli.Kitu kingine alichokubali ni kufikishwa mahakamani kukabiliana na kesi inayomkabili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 8, itakapoanza kusikilizwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...