Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Mbunge wa Donge Visiwani Zanzibar, Sadifa Juma Khamis ambaye alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2012.

Akizungumza leo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamidu amesemma wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM linafanya usahili wagombea waliomba nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema usahili huo unafanyika kwa waliomba kugombea wa nafasi za mwenyekiti, makamu, wajumbe watano wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wajumbe wa kuwakilisha jumuiya hiyo katika jumuiya nyingine za chama.

Amesema zoezi hilo ambalo limeanza tangu Aprili limefanikisha kupatikana kwa viongozi mbalimbali wa ngazi za shina hadi wilaya na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za kitaifa.“Vijana 113 wamejitokeza kuomba nafasi ya uenyekiti. Huu utakuwa ni uchaguzi wa kihistoria kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika tangu mwaka 1978 ilipoanzishwa jumuiya hii mwaka huu. Kwa maneno mengine tumevunja rikodi,”amesema.

Amesema kwa upande wa nafasi ya umakamu mwenyekiti waliomba kugombea ni 23 wakati ujumbe wa Nec 118 wanachuana kugombea nafasi tano zilizopo kikatiba.Shaka amesema jumla ya wagombea ambao wanawafanyiwa usahili katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji wa baraza la Kuu la UVCCM ni 375 huku nafasi ya uenyekiti Taifa ikiongoza kwa waombaji wengi katika zoezi hilo.
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...