Zaidi
ya wanahisa 1500 wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Walikutana
kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki na kufanya mkutano na Uongozi wa
kampuni hiyo na kuchagua viongozi mbalimbali na kufikia mwaafaka wa gawio
la kwanza la Hisa kwa wanachama hao utakaotolewa na kampuni hiyo kiasi
cha zaidi ya shilingi Bilioni 26 ifikapo mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Hayo
yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,na Mwenyekiti wa Bodi ya
Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya
waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa gawio hilo kwa wanahisa wake.
Mwenyekiti
huyo wa bodi alisema kwamba kila mwana hisa atapatiwa gawio hilo la shilingi 12
na senti 74.
Aidha
alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na kuimarika vizuri kwa
kujiendesha kibiashara hivyo iliona ni vyema kutoa gawio hilo, ili kila
mwanahisa aweze kunufaika pale inapobidi.
Kampuni
hiyo pia iliweza kufanya mkutano wake Mkuu wa mwaka kwa kuwakutanisha wanachama
wake kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kwenda
sambamba na uteuzi wa wajumbe wapya watakaoingia ndani ya bodi ya wakurugenzi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ian Ferrao aliwapongeza
wajumbe wote walioteuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha
hisa za vodacom zinaleta manufaa kwa wamiliki wake wote.
“Wanahisa
watoe shaka kabisa kuhusiana na hisa zao kwani zipo salama na kampuni
inaendelea kufanya vizuri sokoni na ninawapongeza wajumbe walioteuliwa na
ninaimani nayo kwani itafanya kazi kwa kushirikiana vizuri na
wanachama ndani nasi tutawapa ushirikiano wakutosha ndani ya kampuni
yetu”, alisema Ferrao.
Mkutano
huo mkuu wa mwaka umefanyika kwa mara ya kwanza kwa wanachama wake tangu
kampuni hiyo iuze hisa zake kwa Umma.
Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC
wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao
uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC
wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao
uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wanahisa za
Vodacom Tanzania PLC ,akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa
wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanahisa za
Vodacom Tanzania PLC,wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kulia)wakati wa mkutano mkuu wa kwanza
wa wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa bodi ya
Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanahisa wa
kampuni hiyo, Adella Kaale,wakati wa Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa
hao uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari( hawapo pichani) juu ya Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa
kampuni hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki, Katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Ali Mafuruki
na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Jacgues Marais
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...