ikiwa benki ya Exim ina Mradi unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali hapa nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.Mashuhuda wa msaada huo unavyotolewa ni Mwenyekiti wa bodi wa hospitali Dodoma
Job Lusinde na Daktari mkuu wa Mkoa wa Caroline Damian.
Daktari wa Mkoa wa Dodoma,Caroline Damian akizungumza mara baada ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma kupokea msaada wa Vitanda na magodoro 40 za hospitali za Mkoa hou ikiwa Exim Bank Tanzania ikiwa kwenye mradi wa kupunguza upungufu wa vitanda na magodoro katika hospitali za hapa nchini.
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania mara baada ya kukabidhi magodoro na vitanda 40 katka hospitali za mkoa wa Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge akisikiliza kwa makini
HOSPITALI
na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na
vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Kama sehemu ya kampeni yake
yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Benki ya Exim
Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa
iliyoko Dodoma.
Benki
ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka
huu, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali
jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania. Mradi
huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini -
hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za
serikali katika mikoa 13 nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana
Stanley Kafu alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu
sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa
miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya
afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika
kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza
katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Bilinith Satano Mahenge alipongeza Exim Bank
Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma
hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali
ya rufaa ya Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...