Picha juu na chini ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (wa tano kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa sita kushoto) kwa pamoja wakizindua Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Mwanza iliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP. 

Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu na Mtaalamu wa Miradi UNDP Tanzania, Amon Manyama (wa nne kushoto), Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel Nyantahe (wa tano kushoto), Kamishna wa Jeshi la Polisi Bw. Clodwing Mtweve (wa pili kulia) pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini na wa mkoa wa Mwanza katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella na meza kuu wakionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za jiji la Mwanza huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...