Katika jitihada za kuchagiza maendeleo ya kilimo Visiwani Zanzibar, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya ziara katika miradi mbalimbali ya kilimo visiwani humo.
Ziara hiyo imelenga kufanya utambuzi wa miradi ambayo ina uhitaji wa mikopo ya gharama nafuu hali itakayochochea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma (aliyesimama) akizungumza na ugeni huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi hiyo, Bibi Rehema Twalib, amesema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
“Ziara yetu hii inalenga katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” alisema.
Akaongeza kuwa lengo la TADB linasadifu majukumu ya kuanzisha kwa ZSTC ambayo yanalenga kuchagiza maendeleo katika mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika mazao ya ili kilimo hivyo kukuza, kuboresha ubora na kuongeza ushindani wa kupamba na bidhaa nyingine za kilimo katika soko la dunia.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa ujio wa TADB visiwani Zanzibar utasaidia kutatua tatizo la mitaji kwa wakulima kwani kwa sasa taasisi za nyingi za fedha zinaelekeza mikopo zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa.
“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa na kuwasahau wakulima na wasindikaji wa mazao, hivyo tunaamini TADB itasaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Ziara hiyo imelenga kufanya utambuzi wa miradi ambayo ina uhitaji wa mikopo ya gharama nafuu hali itakayochochea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma (aliyesimama) akizungumza na ugeni huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi hiyo, Bibi Rehema Twalib, amesema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
“Ziara yetu hii inalenga katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” alisema.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bibi Rosebud Kurwijila,
Bibi Rehema Twalib, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki
hiyo (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao na uongozi wa ZSTC.
Akizungumza na ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma alisema ujio wa TADB visiwani humo kutasaidia wakulima wa Zanzibar ambao kama walivyo wakulima wengine nchini kukosa mikopo ya gharama nafuu hali inayorudisha nyuma jitihada za wakulima hao.Akaongeza kuwa lengo la TADB linasadifu majukumu ya kuanzisha kwa ZSTC ambayo yanalenga kuchagiza maendeleo katika mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika mazao ya ili kilimo hivyo kukuza, kuboresha ubora na kuongeza ushindani wa kupamba na bidhaa nyingine za kilimo katika soko la dunia.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (alyesimama)
akifafanua kuhusu malengo ya TADB wakati wa mazungumzo yao na ZSTC.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini,
Zanzibar.
Bw. Juma akaahidi ZSTC kutumia ushirikiano huo na TADB katika kuwezesha maendeleo na kusaidia mabadiliko ya sekta ya kilimo visiwani humo.Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa ujio wa TADB visiwani Zanzibar utasaidia kutatua tatizo la mitaji kwa wakulima kwani kwa sasa taasisi za nyingi za fedha zinaelekeza mikopo zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa.
“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa na kuwasahau wakulima na wasindikaji wa mazao, hivyo tunaamini TADB itasaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...