Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya
ujenzi wa zahanati wenye thamani ya Shilingi Milioni 14.7 za Kitanzania
kutoka Darworth Ltd, Mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji matunda, kama
shukurani baada ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya
ujenzi wa kiwanda hicho Kitongoji cha Mkomba katika Kijiji cha
Michungwani Wilayani Handeni..
Akizungumza wakati wa mapaokezi ya vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuhakikisha wanasimamia na kutumia vifaa kwa kadri ilivyokusudiwa na kwamba asitokee mtu yeyote kupindisha matumizi au kusimamisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Ameongeza kuwa yote hayo yanafanywa kwaajili ya wananchi wa Handeni na kwamba maendeleo hayana itikadi, hivyo roho ya maendeleo iliyopo waishikilie ili wasonge mbele kwa pamoja kwakuzingatia kuwa wanatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
Gondwe amesema kuwa Mh.Rais ameagiza kuwepo kwa maeneo yanayotengwa rasmi kwaajili ya viwanda , na sisi kama viongozi tumejumuika kwa pamoja kusimamia agizo la Mh.Rais, kwa Handeni ni wajibu wetu kuhakikisha tunaendelea kutenga maeneo kwaajili ya viwanda kama ambavyo kiwanda hiki kitakavyojengwa.
“Asitokee mtu akauondoa umoja huu, huu ni mwanzotu, viongozi tunakazi ya kuhakikisha vifaa hivi vilivyoletwa vinafanye kazi yake na wananchi waone matunda ya rasilimali yao” amesema Gondwe
Kadhalka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameahidi kusimamia na kuhakikisha vifaa vyote vinatumika ipasavyo na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji ili kufikia malengo ya ukamilishaji wa kiwanda cha kusindika matunda.

wa Wilaya ya Handeni MH. Godwin Gondwe (mwenye koti jeusi akipokea
nondo kutoka kwa mwekezaji John Kessy kwa ishara ya kupeana mikono na
viongozi wengine wakishuhudia
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni kulia name Mwekezaji upande wa Kushoto akipokea
mfuko wa saruji kuwakilisha mifuko mingine ,pembeni ni viongozi
mbalimbali wa Halmashauri
Mapokezi
ya mabomba kwa ajili ya kusambazia maji, Mkuu wa Wilaya ya Handeni
mwenye koti jeusi akipokea kutoka kwa mwekezaji John Kessy, kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na uongozi wa Kata kwenye ofisi ya Kijiji cha Michungwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...