Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
WILAYA ya Kibondo inakabiliwa na upungufu wa vituo vya Afya, ambapo katika Wilaya nzima kuna vituo vya afya viwili hali inayopelekea Wananchi wa Wilaya ya Kibondo kukosa vituo vya kwenda kutibiwa na kupelekea ongezeko la vifo kwa Wananchi kutokana na kukosa huduma.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura amewaagiza Madiwani kuhakikisha wanawahamasisha Wananchi katika kata zao kuibua vituo vya Afya kwa kuanzisha ujenzi Wa vituo hivyo na Halmashauri kumalizia ujenzi huo ili kuhakikisha vituo vya Afya katika Wilaya hiyo vinaongezeka.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Juzi Mkuu huyo alisema jambo la aibu sana kwa Wilaya hiyo kuwa na vituo vya Afya viwili na halmashauri isipochukua hatua ya kurekebisha vituo hivyo vitarudi kuwa zahanati, na amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuhakikisha anaongeza mbinu ya kuibua vituo hivyo angalau Wilaya hiyo kuwa na vituo 10 kwa kuanzia.
Aidha Bura alisisitiza Madiwani kupatiwa Vitambulisho vya bima ya afya ili na wao waweze kuwahamasisha wananchi kuchangia mfuko wa bima ya Afya (CHF) na waweze kupatiwa matibabu bure na kupunguza gharama za matibabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...