Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma jana kwa ajili ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera
mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha
sekta hiyo.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
“Natoa agizo mchakato
huu ukamilike ndani ya mwezi huu wa 11, tarehe moja mwezi wa 12 mlete rasimu
ambayo nyie wataalamu mmeridhika nayo, muiwasilishe kwangu mimi na Mhe. Naibu
Waziri, na siku hiyo mtakayoiwasilisha kwetu mniletee timu ya wataalamu watakaonishauri
kwenye maeneo mbalimbali.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza kukamilishwa haraka kwa rasimu mpya ya
Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 2016 ili kuwezesha upatikanaji wa Sera, Sheria
na Kanuni mpya za usimamizi wa rasilimali za misitu nchini kwa ufanisi zaidi.
Ameagiza wataalamu wa
Wizara hiyo kukamilisha rasimu hiyo mwezi huu wa Novemba na iwasilishwe kwake mapema
mwezi ujao (Desemba) ili aweze kupata ushauri zaidi wa wataalamu wengine huru kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na baadaye kutungiwa Sheria na Kanuni za
utekelezaji.
Dk. Kigwangalla ametoa
agizo hilo jana mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa
misitu iliyolenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki,
pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
“Pamoja na hao wataalamu
washauri nataka watu wengine huru wahusike kwenye kunishauri, ili nipate picha
ya watu wengine huru kabla hatujatengeneza andiko ambalo tutalipeleka kwenye kikao
cha baraza la Mawaziri, waje wanishauri maeneo yanayotaji maboresho, kuongeza ubunifufu
au kukazia zaidi”. Aliagiza Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu majiko banifu ya mkaa muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Alisema amelazimika
kuharakisha zoezi hilo ili Sera hiyo ikamilike haraka iweze kushughulikia changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo ongezeko la watu linalosababisha misitu
mingi kuteketezwa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kupitia
shughuli za kilimo na uanzishwaji wa makazi mapya.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...