Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni umekabidhi matrekta manne (4) kwa vikundi vya uzalishaji na kuvitaka vikundi hivyo kutumia matrekta hayo kwa lengo la kuchochea kasi ya maendeleo ya kilimo kwenye maeneo yao. 

Akikabidhi matrekta hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa amewaeleza vikundi kuwa Halmashauri imeamua kuwapa matrekta hayo kama mtaji kutokana na utayari wa vikundi vyenyewe kwani vikundi vipo vingi ambavyo vingeweza kupewa na hivyo watambue wanao wajibu wa kuyatunza na yasiwe chanzo cha migogoro.

Amesema kuwa Halmashauri inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kuhudumia wananchi, matrekta yaliyotolewa wangeweza kutoa hata kwa mtu mmoja mmoja lakini yametolewa kwa vikundi ili kuchochea maendeleo na kurahisisha utunzaji wa mradi huo. 

“kasaidianeni matrekta haya yakachochee na kuboresha kilimo, kuongeza uzalishaji na tija asitokee mtu mmoja kati yenu akawa ni chanzo cha mafarakano, Halmashauri haitavumilia tutawapokonya na kuwapa wahitaji wengine” alisema

Ameongeza kuwa matrekta yote matengenezo yake yapo chini ya Suma JKT hivyo iwapo kutatokea hitilafu yoyote wasitumie mafundi wa mitaani kuyatengeneza badala yake yafikishwe kwa walengwa wa matengenezo, na kuwataka wasitumie mradi huo kwa lengo la kujinufaisha mtu binafsi. 
Mwenyekiti wa Halmashauri MH Ramadhani Diliwa akimkabidhi Kiongozi wa kikundi cha umoja wa marafiki Mkata  nakala za mkataba .

 Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani Diliwa wa tatu kushoto akizungumza na vikundi juu ya usimamizi bora wa matrekta hayo kwa lengo la kuchochea matumizi ya zana bora zakilimo
 Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani diliwa akijaribu kuwasha trekta mojawapo Kama ishara ya majaribio baada ya matengenezo.
 Muendeshaji wa trekta aliyeshika usukani wa trekta akitoa ufafanuzi wa vitendo kwa Mkurugenzi Mtendaji William Makufwe mwenye shati jeupe juu ya namna ya uendeshaji wa trekta hilo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...