Na Bashir
Yakub.
Kuna mambo ambayo yafaa
tujihadhari nayo sana
hasa kipindi hiki. Wengi wamefutiwa umiliki wa
ardhi. Takwimu za kufutiwa ni
kubwa sana kipindi hiki kama ulikuwa hujui. Kwa
watu wanaonunua ardhi
na kwenda kuishi
nje ya nchi
hili lawahusu sana kabla hamjapoteza ardhi zenu.
Najua unachojua
kuhusu kutelekeza ardhi ni pengine
kutokujenga, au kutoitumia
kama ilivyopangiwa matumizi, nk. Ni kweli lakini hiyo ni maana
finyu ya kutelekeza ardhi.
Maana ni
zaidi ya hiyo, na hapa tutaona
ili ujihadhari na uwezekano wa
kupoteza ardhi yako.
1.MAMBO AMBAYO
UKIFANYA UTAHESABIKA KUTELEKEZA
ARDHI.
Mambo haya yameelezwa
na Sheria Namba
4 ya ardhi
ya 1999 kifungu cha
51(1).
( a ) Kutokulipa kodi, tozo
au ushuru wowote
ambao upo kisheria
kwa ajili ya
ardhi ni kutelekeza
ardhi kwa mujibu
wa sheria hiyo. Mnazijua
kodi za majengo,
kodi za ardhi
nk. Hizi ni
muhimu sana na kimsingi ndizo
zinazoeleza uhai wa
ardhi yako.
Ikiwa hulipi hizi hata
kama eneo hilo
umejenga kiwanda kinachofanya
kazi saa 24
siku 7 za
wiki bado mbele
ya macho ya
sheria unahesabika kutelekeza
ardhi. Dawa ya
kuepuka hili ni
ndogo. Lipa hizo
kodi na tozo
kwa mujibu wa
sheria. Yamkini hizi huwa si
pesa nyingi sana ya
kumshinda mmiliki kulipa.
( b ) Jengo ndani
ya ardhi kuwa
gofu ni kutelekeza
ardhi kwa mujibu
wa sheria. Lakini
pia katika eneo hilo
sheria imetumia neno “disrepair”. Maana
yake kutokufanya ukarabati.
Kwa tafsiri hii
ni kuwa kumbe
hata kutokufanyia majengo
yetu ukarabati nako ni kutelekeza
ardhi.
Utaona katikati ya
miji yetu majengo ya
zamani machafu, yaliyopauka.
Japo ndani mwake
watu wanaishi na
maofisi yamo bado kwa tafsiri ya
neno “disrepair” ni
kuwa jengo hilo
limetelekezwa. Na sheria
imeeleza zaidi kuwa itakuwa
mbaya zaidi ikiwa
jengo hilo linahatarisha
afya au maisha ya
watumiaji wake , majirani au
hata wapita njia.
KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...