Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Televisheni inayoshughulika na masuala ya filamu za Kitanzania kwa Wasanii wa Bongo Movie JTV, ambayo itapatikana kupitia king'amuzi cha Star Times ambapo amewataka wasanii hao kujiongeza ili wafanye kazi kama wasanii kutoka nchi za Magharibi.
Waziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa Televisheni ya Jtv itakayooneshwa kwenye king'amuzi cha Star Times
Mkurugenzi wa Jtv, Jason Msimbe akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye uzinduzi wa televisheni yake
Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa Tlevisheni mpya ya Jtv ambayo itakuwa inaonesha filamu za kitanzania kupitia King'amuzi cha Star Times
Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiteta jambo naWaziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na Mkurugenzi wa JTv Jason Msimbe
Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Bongo Movie walioshiriki uzinduzi wa Televisheni ya Jtv
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...